Rapa mkongwe kwenye ‘game’ ya Hip hop ya Bongo, Fid Q , ameamua kuwajibu kivitendo watu waliomponda kuwa hana mafanikio yoyote kwenye muziki, kitu ambacho amedai kilimuumiza.

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Fid Q ambaye mara nyingi huwa hapendi kuweka wazi maisha yake binafsi, amesema kwamba kauli ya kuambiwa hana maendeleo yoyote licha ya kuwa na ‘influence’ kwa vijana wengi, ameamua kuwajibu watu hao kivitendo na kuonyesha gari yake aina ya ‘Jeep’, ambayo ina mpaka Dj Set nyuma.

“Kuna kitu kilinigusa sana kwenda kusema kwamba mimi ni msanii mkubwa kwenye Hip hop nina ‘influence’, nawahamasisha vipi vijana waone kama hiki kitu inaleta maana, nikasema sawa labda nikionyesha hii kitu itasaidia kuwaeleza vijana”, amesema Fd Q.

Gari hiyo ya Fid Q, Jeep Cherokee inauzwa dola 33,320 ambayo ni sawa na zaidi ya milioni 76 za Tanzania.