Ikiwa leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwadada aliyewahi kushikiria taji la urembo nchini 2000 Jackline Ntuyabaliwe ambaye pia ni mke wa mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya IPP Bw.Reginarld Mengi,ambapo ndugu jamaa wametumia siku hii kumtakia maisha marefu.

Kylin alipokea ujumbe mzito wa mahaba kutoka kwa mume wake huyo ambaye ni bilionea wa Afrika, ujumbe ulioonesha upendo, mengi amefunguka kupitia ujumbe huo kuwa sababu kubwa ya yeye kuishi ni mke wake kylin.

Naye kylin alionesha kujari kwa kujibu ujumbe huo alioupokea kutoka kwa mume wake kwa kuandika maneno ya shukrani na kusema kuwa hili ni jambo jema na kuwa asingeweza kumuomba mwanaume mwingine bora zaidi ya mengi na kumalizia kwa kusema Mengi ni kila kitu kwake.