Rapa wa kike bongo Chemical ameweka wazi mipango yake ya kujioa, baada ya kuona kashaumizwa sana kwenye mahusiano.

Akizungumzia project yake mpya alipokuwa akizungumza na mwandishi wa kituo cha eatv , Chemical amesema ameamua kuja na idea hiyo kwenye kazi yake anayotarajia kutoa, hivyo watu wakae mkao wa kula kusubiri na kushuhudia jinsi anavyojioa na kujivisha pete.

“Nataka nijioe, nilishaumia ‘thats why’ nataka nijioe, wasubirie waone Chemical anavyojioa na kujivisha pete”. amefunguka.

Hivi karibuni rapa huyo aliweka wazi juu ya maumivu aliyopitia kwenye mahusiano yake, na kuamua kukaa bila kuwa kwenye mahusiano kwa muda.