Baada ya kutoka Uganda, kwa sasa Diamond ameweka majeshi kwa mrembo huyu wa Kenya, ambaye ni mtangazaji wa Kituo cha Luninga cha NRG, aitwaye Natasha.

Diamond inaelezwa kuwa amepagawa na penzi la Tanasha Donna kwa sasa anawaza ndoa tu.

Wiki iliyopita Diamond alipiga shoo moja matata mjini Thika na Tanasha alikuwepo na hapo akatambulishwa rasmi kwa mashabiki kwamba, ndiye mpango mzima kwa sasa.

Pia, Chibu Dangote aliweka bayana kwamba, miongoni mwa wasichana aliowahi kuwa nao amemweleza zaidi Tanasha hivyo, anataka kufuta rekodi zote za nyuma na kutulia na mrembo huyo.

“Tanasha ndiye mwanamke pekee aliyeonesha kujali na uzito juu ya jambo hilo hivyo rasmi natangaza kumuoa huyu. Ana sifa zote za mwanamke wa kuoa, lakini unajua sisi wanaume wengi huwa tunaangalia sura, umbo na vingine vya mwilini kisha ndiyo inafuata tabia. Lakini nimejiridhisha kwamba mbali na umbo na mvuto wa kipekee pia ni mwanamke mwenye tabia nzuri,” Diamond alikiambia chombo kimoja cha habari nchini Kenya alikokuwa wiki iliyopita kwaajili ya show.