Uongozi wa WCB kupitia kiongozi wake ambaye pia ni Msanii wa kizazi kipya Nassib Abdul almaarufu kama Diamond mapema leo wametoa msaada mkoani Sumbawanga wa vifaa vitakavyosaidia kumaliza ujenzi wa shule ametoa mabati 150 pamoja nakutoa bidhaa kwa kila mwanamke zisizopungua kiasi cha shilingi elfu 50000 pamoja na kukabidhiwa shilingi elfu 20000.

WCB wametoa msaada huo walipokuwa katika moja ya matembezi ya kutembelea maeneo mbalimbali katika mkoa huo.

Katika hatua nyingine Diamond amepata fursa ya kuzindua jiwe la msingi la shule hiyo iliyopewa jina la Diamond kama moja ya kumbukumbu ya mchango wake katika kuhakikisha shule hiyo inajengwa.