Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kesho tarehe 09 Desemba, 2018litaadhimisha Sikukuu ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya shughuli mbalimbali na kutoa huduma za Kijamii kwa Wananchi.
JWTZ litatoa huduma za tiba kwa kuwapima Wananchi magonjwa mbalimbali bila malipo.  Zoezi hilo la tiba litafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kesho Jumapili tarehe 09 Desemba 2018 kuanzia saa mbili (2.00) Asubuhi hadi saa nane (8.00) Mchana.
Wananchi wanataarifiwa kujitokeza ili kupima afya zao. Huduma za tiba zitakazotolewa ni pamoja na Ushauri Nasaha na Upimaji wa Virusi vya Ukimwi, Huduma za Mama na Mtoto, Upimaji wa Uzito, Shinikizo la Damu na Kisukari, Afya ya Kinywa na Meno pamoja na Uchangiaji wa Damu Salama.
 Aidha, kutakuwepo na “Press Conference” na Waandishi wa Habari katika viwanja hivyo kesho saa 4:00 Asubuhi.JWTZ linakialika chombo chako cha habari wakati wa “Press Conference” hiyo.