Msanii wa muziki wa Bongo Fleva,  Diamond Platnumz ametangaza siku ya kufunga ndoa na mpenzi wake mpya, Tanasha.

Kupitia mtandao Instagram, Diamond amesema harusi yake na mrembo huyo kutoka Kenya itafanyika tarehe 14 February mwakani 2019.

“Unajua ni kiasi gani naisubiria siku hiyo (siku ya harusi) father. 14/2/2019 siku ya harusi ya simba,”ameandika Diamond kwenye Instagram ambapo alimjibu mdau mmoja aliyehoji kuhusu ndoa.