Habari zisizo rasmi hapa mjini Dar zinasema Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania Awamu ya Nne Mh. Membe amefungua rasmi kesi ya madai ya fidia ya jumla ya Shillingi Billioni 10 za Tanzania dhidi ya Mwanaharakati maarufu nchini Cyprian Musiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Blogu ya hii ya Le Mutuz inafanya kila jitihada zakumpata Waziri huyo wa zamani ili kuthibitisha habari hizi, ingawa mpaka sasa bado hatujafanikiwa lakini tutawafahamisha mara tu tutakapozipata.

Mwanaharakati maarufu nchini Cyprian Musiba, ambaye hivi karibuni alilishitua Taifa kwa tuhuma nzito alizowatuhumu Wanasiasa wengi wa zamani maarufu nchini akiwemo Waziri Membe.